Posts

Showing posts from November, 2021

001 - Mtakatifu, Mtakatifu,Mtakatifu "Holy, Holy, Holy"

 001 - Mtakatifu, Mtakatifu,Mtakatifu "Holy, Holy, Holy" 1 U Mtakatifu! Mungu mwenyezi! Alfajiri sifa zako tutaimba; U Mtakatifu , Bwana wa huruma, Mungu wa vyote hata milele. 2 U Mtakatifu! Na malaika Wengi sana wanakuabudu wote; Elfu na maelfu wanakusujudu Wa zamani na hata milele. 3 U Mtakatifu! Ingawa giza Lakuficha fahari tusiione, U Mtakatifu! Wewe peke yako, Kamili kwa uwezo na pendo.

002 - Twamsifu Mungu "We Praise Thee, O God"

 002 - Twamsifu Mungu "We Praise Thee, O God" 1 Twamsifu Mungu, Mwana wa upendo Aliyetufia na kupaa juu. Chorus Aleluya! Usifiwe, Aleluya! Amin; Aleluya! Usifiwe, utabariki. 2 Twamsifu Mungu, Roho mtakatifu, Akatufunulia Mwokozi wetu. 3 Twamsifu Mwana, aliyetufia Ametukomboa na kutuongoza. 4 Twamsifu Mungu wa neema yote Aliyetwaa dhambi, akazifuta. 5 Twamshe tena, tujaze na pendo. Moyoni uwashe moto wa Roho.

003 - Mungu Atukuzwe "To God Be The Glory"

 003 - Mungu Atukuzwe "To God Be The Glory" 1 Mungu atukuzwe kwa mambo makuu,  Upendo wake ulitupa Yesu, Aliyejitoa maisha yake, Tuwe nao uzima wamilele. Chorus Msifu, msifu, dunia sikia; Msifu, msifu, watu wafurahi; Na uje kwa Baba, kwa yesu Mwana, Ukamtutukuze kwa mambo yote. 2 Wokovu kamili, zawadi kwetu, Ahadi ya Mungu kwa ulimwengu; Wanaomwamini na kuungama, Mara moja wale husamehewa 3 Alitufundisha mambo makuu,  Alihakikisha wokovu wetu, Lakini zaidi, ajabu kubwa, Yesu atakuja na tutamwona.

004 - Jina LA Yesu Salamu "All Hail The Power"

 004 - Jina LA Yesu Salamu "All Hail The Power" 1 Jina la Yesu, salamu! Lisujidieni, Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi mpeni Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi mpeni 2 Enzi na apewe kwenu, watetea dini; Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni 3 Enyi mbegu ya rehema nanyi msifu; Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni 4 Wenye dhambi kumbukeni ya msalabani Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni. 5 Kila mtu duniani msujudieni Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni. 6 Sisi na wao pamoja tu mumo sifani. Milele sifa ni moja, na `mpeni` Milele sifa ni moja, na `enzi mpeni`

005 - Na Tumwabudu Mfalme Mtukufu "O Worship The King"

 005 - Na Tumwabudu Mfalme Mtukufu "O Worship The King" 1 Na tumwabudu  huyu Mfalme, Sifa za nguvu zake zivume; Ni ngao, ni ngome, Yeye milele, Ndizo sifa zake kale na kale. 2 Tazameni ulimwengu huu, Ulivyoumwa, ajabu kuu; Sasa umewekwa pahali pake, Hata utimize majira yake. 3 Kwa ulinzi wako, kwetu Bwana, Twakushukuru, U mwema sana; Hupewa chakula kila kiumbe, Kila kitu kila mahali pake. 4 Wanadamu tu wanyange sana, Twakutumaini wewe, Bwana; Kamwe haupunguiwsako wema, Mkoombozi wetu, Rafiki mwema.

006 - Kumekucha Kwa Uzuri "The Morning Bright Rosy'

 006 - Kumekucha Kwa Uzuri "The Morning Bright Rosy' 1 Kumekucha kwa uzuri. Nafumbua macho; Baba amenihifadhi, Ni wake moto. 2 Bwana niwe leo kutwa Ulinzini mwako; Nisamehe dhambi, niwe Mikononi mwako. 3 Roho wako anikae moyoni daima; Anitakase, nione Uso wako.

007 - Mungu Msaada Wetu "O God Our Help In Ages"

 007 - Mungu Msaada Wetu "O God Our Help In Ages" 1 Mungu Msaada wetu tangu miaka yote; Ndiwe tumaini letu la zamani zote. 2 Kivuli cha kiti chako ndiyo ngome yetu, Watosha mkono wako ni ulinzi wetu. 3 Kwanza havijakuwako nchi na milima, Ndiwe Mungu; chini yako twakaa salama. 4 Na miaka elfu ni kama siku moja kwako; Utatulinda daima, tu wenyeji wako. 5 Bwana msaada wetu tangu miaka yote, Mlinzi wetu na ngome, daima, milele.

008 - Uje Ukombozi "O Hear My Cry"

 008 - Uje Ukombozi "O Hear My Cry" 1 Unisikie ninapolia, Uje. M-kombozi; Moyo wangu hukutazamia, Uje. M-kombozi. Chorus Nimepotea mbali na kwangu, Nimetanga peke yangu; Unichukulie sasa kwako: Uje M-kombozi. 2 Sina pahali pa kupumzika, Uje M-kombozi Unipe raha, nuru, uzima, Uje M-kombozi. 3 Nimechoka, njia ni ndefu Uje, M-kombozi Macho yako kuona nataka, Uje M-kombozi. 4 Bwana daima hutanidharau, Uje, M-kombozi Kilio changu utanijibu, Uje, M-kombozi.

009 - Mwumbaji , Mfalme "My Maker And My King"

 009 - Mwumbaji , Mfalme "My Maker And My King" 1 Mwumbaji, Mfalme, Vitu vyote vyako; Ni kwa ukarimu wako; Ninabarikiwa, Ni kwa ukarimu wako, Ninabarikiwa. 2 Uliyeniumba, Nakutegemea; Sina budi kuzisifu Hisani zako kuu, Sina budi kuzisifu Hisani zako kuu. 3 Nitatoa nini? Kwanza vyote vyako, Upendo wako wadai Moyo wa shukrani, Upendo wako wadai Moyo wa shukrani. 4 Nipewe neema, Niwe na uwezo Wa kuishi kwako, Bwana: Siku zangu,zako, Wa kuishi kwako, Bwana: Siku zangu,zako.

010 - Kristo Wa Neema Yote "Come Thou Fount"

 010 - Kristo Wa Neema Yote     "Come Thou Fount" 1 Kristo wa neema zote imbisha moyo wangu Mifulizo ya Baraka inaamsha shangwe kuu. Unifunze nikupende, nikuandame kote, Moyo wangu ukajaefuraha na tumaini. 2 Namshukuru sana Bwana, aniwezesha huku. Salama aniongoza hata kule nyuumbani. Yesu alinitafuta njiani mbali kwake, Akatoa damu yake nipone hatarini. 3 Kweli mimi mwiwa mkubwa wa neema daima; Wema wako unifunge zaidi kwako Bwana. Ili nisivutwe tena kukuacha, ee Mponya, Nitwalie moyo wangu uwe wako kamili.

011 - Jina La Bwana Li Heri "O For A Thousand Tongues To Sing"

 011 - Jina La Bwana Li Heri "O For A Thousand Tongues To Sing" 1 Sauti zote ziimbe, jina la Yesu li heri ! Sifa za mfalme Mungu, jina la Yesu li heri ! Chorus Jina li heri, jina li heri, jina la Yesu li heri. Jina li heri, jina li heri, jina la Yesu li heri 2 Hofu zote la tuliza, jina la Yesu li heri ! Mwenye dhambi hukubali, jina la Yesu li heri. 3 Huvunja nguvu za dhambi, jina la Yesu li heri. Damu yake hutakasa, jina la Yesu li heri. 4 Sauti yake ni tamu, jina la Yesu li heri. Wakaburini husikia, jina la Yesu li heri. 5 Lugha maelf(u) zitaimba, jina la Yesu li heri. Astahili Mwana-Kondoo,  jina la Yesu li heri.

012 - Msifu Mungu "Praise God From Whom All Blessings Flow"

012 - Msifu Mungu "Praise God From Whom All Blessings Flow" Msifu Mungu wa neema, Enyi viumbe po pote; Wa juu pia sifuni Baba, Mwana naye Roho! Amin!

013 - Yesu Uje Kwetu "Jesus Thou Hast Promised"

 013 - Yesu Uje Kwetu "Jesus Thou Hast Promised" 1 Umetuahidi kwamba wawili watatu , Kwajina lako wakija, Utabariki; Kwa hivi leo twapiga magoti nyumbani pako. Chorus Yesu uje kwetu Utubariki; Yesu uje kwetu Uwe karibu. 2 Umekuwa nasi siku nyingine, Tunakuhitaji mpaka mwisho. Uje Mwokozi, tupe neema; ‘Tusikie Yesu, utubariki. 3 Uje utawale sauti zetu: Nyimbo, nazo sala uziagize; Imani izidi, ikamilike; Pendo liwe safi, na njia nuru.

014 - Nitembee Nawe "O Let Me Walk With Thee"

 014 - Nitembee Nawe "O Let Me Walk With Thee" 1 Nitembee nawe mungu Alivyo tembea Henok; Mkonop wangu uushike: Unene nami kwa pole; Ingawa njia siioni, Yesu nitembee nawe. 2 Siwezi tembea pekee: pana dhoruba mbinguni; Mitego ya miguu, elfu; Adui wengi hufichwa; Uitulize bahari, Yesu nitembee nawe. 3 Ukinishika mkono Anasa kwangu hasara; Kwa nguvu nitasafiri; `Tautwika msalaba; Hata mji wa Sayuni Yesu nitembee nawe.

015 - Nena Mungu "Speak To My Soul"

 015 - Nena Mungu "Speak To My Soul" 1 Nena rohoni Yesu, Nena kwa upole Sema kwangu kwa pendo, "Huachwi upweke." Fungua moyo wangu, Nisikie mara; Jaza roho na sifa, Sifa zako Bwana. Chorus Kila siku unene, Vile kwa upole, Nong`oneza kwa pole wa pendo: "Daima utashinda, Uhuru ni wako." Nisikie maneno; "Huachwi upweke." 2 Nena kwa wana wako, waonyeshe njia,  Wajaze kwa furaha, Fundisha kuomba; Wajifunze kutoa Maisha kamili, Wahimize ufalme, Tumwone mwokozi. 3 Nena kama zamani, Ulipoitoa Sheria takatifu: Niiweke pia; Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu, Mapenzi yoko tena, Daima kusifu.

016 - Ninakuhitaji "Blessed Lord, How Much I Need Thee"

 016 - Ninakuhitaji "Blessed Lord, How Much I Need Thee" 1 Bwana ninakuhitaji! Nimpofu, maskini; Unishike mkononi, Kwako napata nguvu. Chorus Kila saa, kila saa Bwana ninakuhitaji; Kila saa, kila saa, Unilinde kila saa. 2 Univike na mavazi Ya usikivu wako; Nguo zangu ni machafu, Nazitamani zako. 3 Wewe ukiniongoza Nitakwenda salama; Nenda nami siku zote, U nuru na uzima. 4 Na ikiwa m-beleni Sehemu yangu ngumu, Au ikiwa furaha, Unilinde kila saa.

017 - Si Mimi, Kristo "Not I But Christ"

 017 - Si Mimi, Kristo "Not I But Christ" 1. Si mimi, Kristo astahili sifa; Si mimi, Kristo ajulikane; Si mimi, Kristo katika maneno Si mimi, Kristo kwa kila tendo 2. Si mimi, Kristo, kuiponya huzuni; Kristo pekee, kufuta machozi; Si mimi, Kristo, kubeba mzigo; Si mimi, Kristo, hupunga hofu. 3. Kristo pekee, pasipo kujisifu; Kristo pekee, na nisizungumze Kristo pekee, na hakuna kiburi; Kristo pekee, sifa yangu ife. 4. Kristo pekee, mahitaji atoe Si mimi, Kristo, kisima changu; Kristo pekee, kwa mwili na kwa moyo. Si mimi, Kristo, hata milele.

018 - Mwokozi, Kama Mchunga "Saviour, like A Shepherd

 018 - Mwokozi, Kama Mchunga "Saviour, like A Shepherd 1 Mwokozi, kama mchunga Utuongoze leo; Ututume malishoni; Fanya tayari boma. Bwana Yesu, peke yako Umetuvuta kwako. 2 Tu wakouwe rafiki, Uwe mlinzi wetu; Kundi lako ulilinde, Tusivutwe na dhambi; Bwana Yesu, tusike, Tukiomba, samehe. 3 Umetuahidi kwamba Utakubali watu, Utawahurumia na Utawapa neema; Bwana Yesu, tunapenda kuwa wako, mapema.

019 - Msalabani Pa Mwokozi "Down At The Cross"

 019 - Msalabani Pa Mwokozi    "Down At The Cross" 1 Msalabani pa Mwokozi Hapo niliomba upozi, Moyo wangu ulitakaswa, Na asifiwe. Chorus Na asifiwe, Na asifiwe, Alinikomboa kwa damu, Na asifiwe. 2 Chini ya mti msumbufu Niliomba utakatifu, Alinikomboa kwa damu, Na asifiwe. 3 Kwa ajabu nina okoka, Yesu anakaa moyoni; Mtini alinifia, Na asifiwe. 4 Damu ya Yesu ya dhamani Huniokoa makosani; Huniendesha wokovuni, Na asifiwe. 

020 - Mungu Wetu Yeye Mwamba "The Lord's Our Rock"

020 - Mungu Wetu Yeye Mwamba    "The Lord's Our Rock" 1 Mungu wetu yeye mwamba, Kimbilio taabuni; Msaada penye shida ulio karibu sana. Chorus Mwambna wetu kutupumzisha, yu kivuli kuburudisha  Yu Mwongozi katika njia, kimbilio taabuni. 2 Mchana usiku, yule kimbilio taabuni, Hivyo hatutaogopa, kwani yu karibu sana. 3 Iwayo yote, Yeye tu kimbilio taabuni, Twamjua Yeye Mlinzi aliye karibu sana. 4 Mungu wetu Ficho kwetu, kimbilio taabuni, Siku zote uwe Boma lililo karibu sana.

021 - Baba Twakujia "Father, We Come To Thee"

 021 - Baba Twakujia "Father, We Come To Thee" 1 Baba twakujia, Uwe msaada; Uwe kimbilio, twakusihi. Dunia ni giza tukitengwa nawe; Fufariji hapa, Baba yetu. Chorus Baba twakujia, tu dhaifu, usitugeue, tusikie. 2 Salama tulinde, kati ya taabu; Uwe raha yetu mashakani. Roho ya sumbuka, Baba tujalie; Twakuomba sana, tupe nguvu. 3 Neema utupe, tukubali kwako; Moyo wetu Linda, safarini; Tuongoe mbele, tupate kushinda Na kufika ng`ambo, kule kwako.