003 - Mungu Atukuzwe "To God Be The Glory"

 003 - Mungu Atukuzwe

"To God Be The Glory"



1

Mungu atukuzwe kwa mambo makuu, 

Upendo wake ulitupa Yesu,

Aliyejitoa maisha yake,

Tuwe nao uzima wamilele.


Chorus

Msifu, msifu, dunia sikia;

Msifu, msifu, watu wafurahi;

Na uje kwa Baba, kwa yesu Mwana,

Ukamtutukuze kwa mambo yote.


2

Wokovu kamili, zawadi kwetu,

Ahadi ya Mungu kwa ulimwengu;

Wanaomwamini na kuungama,

Mara moja wale husamehewa


3

Alitufundisha mambo makuu, 

Alihakikisha wokovu wetu,

Lakini zaidi, ajabu kubwa,

Yesu atakuja na tutamwona.

Comments