001 - Mtakatifu, Mtakatifu,Mtakatifu "Holy, Holy, Holy"
001 - Mtakatifu, Mtakatifu,Mtakatifu
"Holy, Holy, Holy"
1
U Mtakatifu! Mungu mwenyezi!
Alfajiri sifa zako tutaimba;
U Mtakatifu , Bwana wa huruma,
Mungu wa vyote hata milele.
2
U Mtakatifu! Na malaika
Wengi sana wanakuabudu wote;
Elfu na maelfu wanakusujudu
Wa zamani na hata milele.
3
U Mtakatifu! Ingawa giza
Lakuficha fahari tusiione,
U Mtakatifu! Wewe peke yako,
Kamili kwa uwezo na pendo.
Comments
Post a Comment