004 - Jina LA Yesu Salamu "All Hail The Power" 1 Jina la Yesu, salamu! Lisujidieni, Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi mpeni Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi mpeni 2 Enzi na apewe kwenu, watetea dini; Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni 3 Enyi mbegu ya rehema nanyi msifu; Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni 4 Wenye dhambi kumbukeni ya msalabani Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni. 5 Kila mtu duniani msujudieni Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni. 6 Sisi na wao pamoja tu mumo sifani. Milele sifa ni moja, na `mpeni` Milele sifa ni moja, na `enzi mpeni`
014 - Nitembee Nawe "O Let Me Walk With Thee" 1 Nitembee nawe mungu Alivyo tembea Henok; Mkonop wangu uushike: Unene nami kwa pole; Ingawa njia siioni, Yesu nitembee nawe. 2 Siwezi tembea pekee: pana dhoruba mbinguni; Mitego ya miguu, elfu; Adui wengi hufichwa; Uitulize bahari, Yesu nitembee nawe. 3 Ukinishika mkono Anasa kwangu hasara; Kwa nguvu nitasafiri; `Tautwika msalaba; Hata mji wa Sayuni Yesu nitembee nawe.
Comments
Post a Comment