010 - Kristo Wa Neema Yote "Come Thou Fount"

 010 - Kristo Wa Neema Yote

    "Come Thou Fount"



1

Kristo wa neema zote imbisha moyo wangu

Mifulizo ya Baraka inaamsha shangwe kuu.

Unifunze nikupende, nikuandame kote,

Moyo wangu ukajaefuraha na tumaini.


2

Namshukuru sana Bwana, aniwezesha huku.

Salama aniongoza hata kule nyuumbani.

Yesu alinitafuta njiani mbali kwake,

Akatoa damu yake nipone hatarini.


3

Kweli mimi mwiwa mkubwa wa neema daima;

Wema wako unifunge zaidi kwako Bwana.

Ili nisivutwe tena kukuacha, ee Mponya,

Nitwalie moyo wangu uwe wako kamili.

Comments

Popular posts from this blog

014 - Nitembee Nawe "O Let Me Walk With Thee"

004 - Jina LA Yesu Salamu "All Hail The Power"

005 - Na Tumwabudu Mfalme Mtukufu "O Worship The King"